Na Helena Magabe, Tarime
Madiwani wa Halmashauri ya Tarime Vijijini wameomba Halmashauri kutangaza siku ya malipo ya fedha za kunusuru Kaya maskini (TASSAF) kama wanavyotangaza Halmashauri ya mji Tarime ili kuepuka pesa kubaki bila kuwafikia walengwa.
Hayo waliyasemwa katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya mwaka kilichoketi hapo Jana Septemba 3,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo ni baada ya kuona miongoni mwa fedha zilizobaki mwaka huu bila kutumika ni pamoja na shilingi bilioni 4,336 ambazo kuzikulipwa kwa walengwa wa mfuko huo. ....
Diwani wa Kata ya Kwihancha Ragita Mato ameiomba Halmashauri kuiga mfano wa Halmashauri ya mji Tarime Kwa kutangaza siku ya malipo ya fedha hizo kwenye vituo vyao huku wakisisitiza wapewe fedha zao kwa malipo ya mkononi ili kuepusha usumbufu kwa wale wanaotumia simu za watu kupokea fedha zao.
"Kwa nini msiigie mfano wa Halmashauri ya mji Tarime wale wanatangaza siku ya kulipa malipo ya kunusuru Kaya maskini wanajua wote pia kwanini wasilipwe pesa zao mkononi kwa sababu wengine hawana akaunti na wengine Hana simu wanatumia simu za watu" alisema Mato
DT CPA Andrew Ndaba amesema wataangalia namna ya kuweka matangazo ili kuwafikia walengwa wote na kwamba fedha hizo sinakuja na maelekezo ya malipo licha ya kuwa fedha hizo zimebaki kutokana na walengwa wengine kutokuwepo Kwa maana ya kushindwa kupata fedha kutokana na changamoto mbali mbali.
Amesema fedha hizo hutolewa kwa makundi mawili ,kundi la kwanza la kwanza ni la kaya zote maskini na kundi la pili ni la wanufaika ambao wamepewa nguvu na Serikali ili wenye nguvu na uwezo wafanye kazi kwenye miradi lakini wanalipwa fedha zao kupitia akaunti zao na simu zao.
Kwa upande mwingine Mganga mkuu wa Halmashauri hiyo Dk Amin Vasomana amewaomba Madiwani pale wanapopata nafasi ya kuzungumza na Wananchi kupitia mikutano wawahamasishe kuchukua tahadhari ya ugonjwa hatari wa Mpox unaoambukizwa kupitia virusi .
Amesema ugonjwa huo ni hatari lakini Wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari kama zile za COVID kwa njia zake maambukizi nyingi zinafanana na za COVID hivyo amewaomba wananchi kutakasa mikono Yao mara Kwa mara ,kuepuka kula mizoga inayodhaniwa kufa Kwa Mpox,kuepuka kusalimiana Kwa kugusana mikono na kuacha kupiga chafya ovyo.
Akijibu swali la Diwani wa Kata ya Nyarero John Mhabasi ambaye yeye alitaka kujua juu ya ugonjwa wa homa ya ini na jinsi unavyoambukizwa alisema ugonjwa huo umegawanyika mara tatu hapetitis A,B na C lakini A na C mtu anaweza kupata na kupona lakini Hapetitis B nibaya sana mtu akiipata itamsumbua na pale mtu anapoambukizwa virusi vyake ukimbilia kuathiri ini ila chanjo ipo kwa mtu ambaye hajaambukizwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri Simon Kilesi amewaomba Madiwani kupima homa hiyo na kupata chanjo kwani ni tishio kubwa huku akimpongeza Mhe John Mhabasi Kwa kuuliza swali juu ya homa ya ini kwani ni ugonjwa hatari ambao hivyo ametumia nafasi kuwasisitiza Madini kuwa makini.