WALIOMCHINJA MELEMBE WA GGM NAO "WACHINJWA"

GEORGE MARATO TV
0


Mahakama Kuu Kanda ya Geita imewahukumu watuhumiwa watatu kunyongwa hadi kufa baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la mauaji ya Milembe Suleiman (43), aliyekuwa mfanyakazi wa mgodi wa dhahabu Geita(GGML).

Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Mfawidhi Kelvin Mhina katika kesi namba 39 ya mwaka 2023, baada ya mahakama kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri bila kuacha shaka yoyote.


Waliohukumiwa ni Dayfath Maunga (30), Safari Lubingo (54), na Genja Deus, ambao walitiwa hatiani kwa mauaji hayo yaliyotokea mnamo mwaka 2023. Hata hivyo, mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo, Musa Lubingo, ameachiwa huru baada ya mahakama kutomtia hatiani.

Katika hukumu yake, Jaji Mhina ameelezea kuwa mahakama imejiridhisha bila shaka kuwa washtakiwa watatu walihusika katika mauaji ya Milembe Suleiman, na hivyo wanastahili adhabu ya kifo kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ulionekana kuwa thabiti na wa kutosha kumtia hatiani kila mshtakiwa aliyepatikana na hatia.

Baada ya hukumu, wakili wa utetezi Laurent Bugoti ameelezea namna walivyopokea hukumu hiyo.huku Ndugu wa marehemu, Ibrahimu Negena, ambaye ni kaka wa Marehemu Milembe Suleiman, amesema familia yao imepokea hukumu hiyo kwa hisia mchanganyiko. Wakati wanafurahia kuona haki imetendeka, pia wanakumbuka kwa uchungu upotevu wa mpendwa wao.

Hukumu hii imeonyesha tena msimamo wa mahakama za Tanzania katika kutoa adhabu kali kwa makosa ya mauaji, ikionyesha kuwa haki itatendeka bila kujali hali ya mshtakiwa. Kesi hii pia inaashiria changamoto zinazowakabili wanasheria wa utetezi katika kuhakikisha kuwa wateja wao wanapata haki wanayostahili.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top