Kati ya miili hiyo, miwili imetambuliwa ambapo mmoja ni wa Gedion Samwel Mnyawi (53), aliyeuawa baada ya kuwauzia shamba mara mbili Hawa Hussein Sumwa (54) na Idd Hussein Idd (25) wote wakiwa wakazi wa Makuro.
Akitoa taarifa hiyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime amesema baada ya watu hao kuuziwa shamba hilo mara mbili na baadaye kugundua kuwa shamba hilo tayari liliuzwa kwa mtu mwingine, walikwenda kwa mganga huyo ambaye aliwaambia kuwa ili pesa zao zirudi inabidi mwanaume huyo atolewe kafara.