Na Helena Magabe -Tarime
Diwani wa Kata ya Kenyamanyori Mhe Farida Joel amechagulia kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira kwa mwaka 2024 ni baada ya kufanyika uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti pamoja na kamati ndogo ndogo.
Kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti kwenye kamati hiyo huwenda kile kilio chake cha muda mrefu cha uchafu kutelekezwa kwenye mtaa wa kibaga mine kikaisha Kwa sababu idara ya afya iko chini ya kamati hiyo ya mipango miji na mazingira hali kadharika Tarura.
Kabla ya Mheshimiwa huyokuchanguliwa kuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo amehoji uchafu utaendelea kuishi kwenye mtaa wa kibaga mine hadi lini na mtaa huo utafikiwa lini na gari la taka kwani imekuwa kero ya muda mrefu ambayo amekuwa akiilalamikia bila kupata majibu ya kina.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji ambaye ni Diwani wa Kata ya Nyamisangura amechaguliwa tena kuendelea kubaki kuwa Makamu Mwenyekiti huku Kata yake ikiwa na kero sugu ya dampo lilipo katikati ya makazi ya watu ambalo amekuwa akipiga kelele liondolewe bila mafanikio.
Diwani wa Kata ya kitale Daudi Wangwe(Ngamia) amesema swala la usafi ni la kila Mtu anapaswa kushiriki na swala hilo litakuwa rahisi endapo Watendaji watafafuatilia kwa karibu lakini wakiachiwa madiwani peke yao hawateweza.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Tarime Daniel Komote ambaye ni Diwani wa Kata ya Nkende ametoa siku Saba dampo Kwa Afisa Afya Erasto Mbunga kuhamisha dampo mtaa wa mwangaza Kata ya Nyamisangura na kuhamishiwa eneo jipya lililotengewa katika Kata ya Nkende kwani bajeti yake ya shilingi milioni 20 imekamilika.
Komote amewashukuru waandishi wa habari kwa kuwa mstari wa mbele kutangaza mnaendeleo ya Halmashauri na kuachana na zile zilizokuwa zinachafua mji wa Tarime ,amelishukuru Jeshi la polisi Kwa kuimarisha ulinzi na usalama pamoja na wadau wengine .







Comments
Post a Comment