Mwonekano wa Ujenzi wa Daraja la John Pombe Magufuli (Kigongo - Busisi) Kilometa 3.2 linalojengwa kuunganisha Barabara Kuu ya Usagara - Sengerema - Geita kupita Ziwa Victoria Mkoani Mwanza na ujenzi wa barabara unganishi ya Kilometa 1.66 utekelezaji unaendelea na upo asilimia 90.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ujenzi Kupitia mtandao wa X zamani uliokua unajulikana kama (twitter) inaeleza kuwa mradi huo unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa shilingi Bilioni 716.3 zikijumuisha Malipo ya Mkandarasi, Mhandisi Mshauri wa usimamizi wa mradi, Fidia na Usanifu.
(Picha Kwa Hisani ya Wizara ya Ujenzi)





Comments
Post a Comment