Serikali kupitia wizara ya afya imepunguza rufaa za nje ya nchi kwa asilimia 97 ikiwa ni matokeo ya uwekezaji uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hayo yamesemwa Agosti 11, 2024 Mkoani Kilimanjaro na Naibu waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati wa mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii na viogozi wa kata 170 katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali.
Aidha Dkt. Mollel amesema kuwa Serikali imewekeza teknolojia ya kisasa katika Hospitali zote nchini ikiwa ni kutekeleza uboreshaji wa huduma za afya kwa jamii ili kila mwananchi apate huduma bora za afya.
"Tumepunguza rufaa za nje kwa asilimia 97, wanaokwenda nje kwa ajili ya matibabu ni asilimia 3 huu ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais Wetu ameleta hospitali nzuri na vifaa tiba vya kutosha ili kuleta huduma bora kwa wananchi". Amesema Dkt Mollel.






Comments
Post a Comment