Na Shomari Binda-Musoma
MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Mhe. Vedastus Mathayo ametoa wito na kushauri bodaboda wanafanya shughuli zao maeneo ya utoaji wa huduma za afya Manispaa ya Musoma Kufanya Kazi kwa ushirikiano
Mhe Mathayo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na bodaboda wanaopaki kwenye hospital ya manispaa Musoma katika ziara yake ya mtaa kwa mtaa.
Amesema ameshangaa kusikia Bodaboda hao wanapopeleka abiria kwenye hospital ya rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kwangwa wanazuiliwa kupaki na kuondoka na abiria huku wote wanatoa huduma kwa jamii hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa kushirikiana na kupendana
Mathayo amesema sio vyema kubaguana kwa kuwa shughuli yao ni moja na yule anayepaki hospital ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere anaweza kupaki hospital ya manispaa ya Musoma.
" Nimesikia hii changamoto ni jambo la kuzungumzika na kazi ikafanyika kwa kushirikiana kwa kuwa wote mnafanya kazi kwa wananchi wetu.
Nimempigia simu mganga mfawidhi pale hospital ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ameniambia hakuna shida yoyote juu ya hilo naomba tukae na kufanya kazi kwa pamoja"Amesema.
Kwa upande wa bodaboda wanaopaki hospital ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wamesema hakuna tukio la kubaguna bali viongozi wao wanapaswa kukutana na kuzungumza jambo Hilo.

Comments
Post a Comment