Na Angela Sebastian
WAZIRI wa habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Mnauye ameagiza Shirika la umeme nchini Tanesco na Wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) kupeleka huduma za umeme na barabara maeneo yote yanapojengwa minara ya mawasiliano.
Amesema hii itasaidia wadau hao kukabiliana na changamoto kadha wa kadha ikiwemo kuingia gharama za manunuzi ya petrol na diseli kuendesha mitambo minara hiyo.
Nape amesema.hayo baada ya kuwasili mkoani Kagera kwa ziara ya siku moja kupokea taarifa ya mkoa na chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo inaonesha kuimalika kwa mawasiliano mkoani humo.
Amesema kuwa agizo la kupeleka huduma hilo ni la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwamba Tarura,Rea na Tanesco wahakikishe wanafikisha huduma hizo maeneo inapojengwa miundombinu ya minara kama ilivyo katika taasisi nyingine kama vile shule na hospitali na maji.
Amesema makadilio ya kuendesha mnara kwa kutumia dizeli kwa ni makubwa na kutumia fursa hiyo kupongeza makampuni ya simu ikiwemo Tigo na Vodacom kwa uwekezaji wao hususani katika minara ya simu ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya mawasiliano.
"Mawasiliano ni uchumi huduma za mawsiliano zikikosekana huduma mbalimbali zinakata mfani Serikali haikusanyi hivyo haya ni maeneo ya kimkakati tusaidieni kufikisha huduma.hizi"anasema Nape
Ameshauri uongozi wa mkoa huo kusaidia makampuni hayo kutatua changamoto wanazokumbana nazo katika maeneo wanayojenga minara ikiwemo masuala ya wananchi kuitaji fidia kubwa na migogoro ya wananchi na wawekezaji hao kuhusu masuala ya ardhi.
Ameongeza kuwa tangua kuanzishwa kwa mpago huo wa kidigitali mkoa wa imepangiwa kujengwa minara 45 na mpaka sasa minara kumi imekamilika ambapo jumla ya shillngi bilioni 6.6 imetengwa na Serikali kama ruzuku ya kuunga mkono juhudi za wadau na ikikamilika itanufaisha watu zaidi ya watu laki moja.
Naye kaimu mkuu wa mkoa ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Bukoba Elasto Sima amesema wasiliano katika mkoa huo yameimalika kwa kiasi kikubwa.

Comments
Post a Comment