Na Emmanuel Chibasa
Habari za uongo na uzushi ni miongoni mambo yanayoisumbua dunia kwa sasa. Wanao kutiana na changamoto hii ni watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwa ni kupata habari au shughuli za kibiashara.
Kuna aina mbalimbali za habari za uzushi na uongo ambazo hatumika zaidi kwenye mitandao ya kijamii kama vile facebook na YouTube ambapo kichwa cha habari hutofautiana kabisa na maudhui ya habari yenyewe au kichwa cha habari pekee bila ya kuwa na maudhui ya habari katika kueleza zaidi juu ya habari husika.
Mara nyingi madhumuni ya upotoshaji huo ni watu kutaka kujipatia pesa kwa njia ya matangazo au kujiongezea watazamaji na wasomaji. Lakini habari au taarifa huzo hutumika kuharibu heshima na sifa ya watu kwenye jamii.
Kwa mujibu wa takwimu za mawasiliano ya robo ya mwaka inayoishia machi 2024 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Tcra), Idadi ya laini za internet imeongezeka kutoka milioni 35.9 kwa robo mwaka iliyoishia desemba 2023 hadi milioni 36.8 kwa robo mwaka iliyoishia machi 2024.
Kutokana na idadi ya watumiaji wa internet kuzidi kuongezeka ni wazi kwamba pia kumekua na mwamko mkubwa wa matumizi ya data, simu janja pamoja na teknolojia.
Mitandao ya kijamii imejitokeza na kuendelea kuwa vyombo vya habari vya kusambaza habari na taarifa mbalimbali na kwa mifumo mbalimbali. Lengo likiwa ni kupata habari na tarifa zilizo sahihi na watumiaji wa mitandao ya jamii wanapaswa kujilinda dhidi ya habari na taarifa za uongo na uzushi.
Kadri matumizi ya teknolojia yanavyozidi kushika Kasi Watumiaji wa internet wanaotegemea mitandao kama vyanzo vya habari au taarifa wanaweza kutambua iwapo habari na taarifa wanazozisoma, kuzisikiliza au kuziona ni za uongo, uchochezi, uzushi au za kutusi watu waengine.
Kama mtumiaji wa mitandao ya kijamii unawezaje kugundua iwapo habari ni ya kweli au sio ya Kweli kwenye mitandao ya kijamii? Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imekuandalia muongozo unaokuwezesha kuangalia vitu ili kubaini habari za uongo na uzushi katika mitandao ya kijamii kama vifuatavyo:
1.Kuwa na Mashaka na Vichwa vya Habari Vyenye Mbwembwe;
Habari nyingi za uongo zinakuwa na vichwa vya habari vilivyoandiskwa kwa maneno na mpangilio unaoonyesha mbwembwe, na iwapo utaona kichwa cha habari chenye maneno ambayo kwa harakaharaka unashuku ukweli wake, upo uwezekano mkubwa kwamba habari hiyo sio ya kuaminika.
2.Angalia Vizuri Anwani ya Tovuti Inayotumika;
Kila tovuti ina anwani inayotambulika kimataifa na inaanza na herufi ‘www’. Angalia kwa makini anwani ya tovuti husika kama ni ya kuaminika. Iwapo habari ipo kwenye anwani ya uongo au ambayo imeghushiwa, basin i dhahiri kwamba habari yenyewe sio ya kuaminika.
Mitandao mingi yenye habari za uongo inatumia anwani ambazo kwa harakaharaka unaweza kudhania kwamba ni za mitandao ya habari inayoaminika. Ukiona huli, tembelea anwani ya uhakika na linganisha na ile yenye habari unayoishuku.
3.Chunguza Chanzo cha Habari;
Hakikisha kwamba habari imeandikwa na mwandishi ambaye unamwamini kwamba ana sifa ya kuandika ukweli. Kama habari inatokana na taarifa za taasisi ambayo huifahamu, chukua hatua za kujiridhisha.
4. Angalia Usanifu au Mpangilio Usio wa Kawaida;
Tovuti nyingi za kugushi zinakuwa na mpangilio wa manno na usanifu usio wa kawaida na unatakiwa kuwa macho ukiona dalili hizo.
5. Angalia Vizuri Picha;
Mara nyingi habari za uongo zinakuwa na picha za kawaida na za video ambazo zimechakachuliwa. Inawezekana picha au video vikawa ni vya kweli lakini vikawekwa kwa mpangilio ambao unaleta maana tofauti na ile ya awali. Ukiona hili tafuta chanzo cha picha ili kuhakikisha ilikotoka.
6.Kagua/Chunguza Tarehe;
Habari za uongo zinaweza kuwa na tarehe ambazo hazina mantiki au hata tarehe ambazo zimebadilishwa.
7.Thibitisha vyanzo vya habari;
Chunguza vyanzo vya mwandishi wa habari husika ili kuthibitisha uhakika. Habari ambayo haina maelezo ya kuthibitisha uhalisia wake au inanukuu wahusika ambao hawatajwi ina kila dalili ya kuwa habari hiyo ni ya uongo.
8.Linganisha na Taarifa za Vyombo Vingine;
Iwapo hakuna chombo kingine chochote kinachotoa taarifa hiyo, ni dalili kwamba habari hiyo ni ya uongo. Habari iliyoandikwa na vyombo vingi ina kila dalili ya kuwa ni ya kweli.
9.Je Habari Hiyo ni Utani;
Wakati mwingine inakuwa vigumu kutofautisha kati habari za uongo na utani, vichekesho au dhihaka. Thibitisha iwapo chanzo cha habari hiyo kinajulikana kwa vichekesho na iwapo habari yenyewe imeandikwa kwa namna ambayo inaonyesha kwamba suala linalozungumziwa ni la kufurahisha tu.
10.Habari Nyingine Zinakuwa za Uongo Makusudi;
Soma habari kwa namna ambayo unaipima ukweli wake na usisambaze kwa wengine habari ambayo unatambua kuwa sio ya kuaminika na Kila habari unayoiona Kupitia Simu au computer lazima uisambaze na tukifanya hivi kwa pamoja tunaweza kuondoa usambazaji wa habari za uongo.
Chanzo: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(Tcra)

Comments
Post a Comment