Naibu Katibu Mkuu , Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila amefurahishwa na viwango vya ujenzi wa miradi ya barabara za lami zinazosimamiwa na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoani Dodoma.
Mhandisi Mativila ameyasema hayo mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya kukagua uimara wa barabara zinazosimamiwa na TARURA ambapo alitembelea miradi ipatayo nane.
Alisema barabara zote hizo zimejengwa kwa fedha za tozo na mfuko wa maendeleo wa barabara ambazo hutolewa na serikali kwaajili ya kuboresha miundombinu ya barabara hususani maeneo ya mijini.
“Nimefurahishwa na viwango vya barabara hizi ambazo zinasimamiwa na TARURA pamoja na makandarasi waliojenga barabara mkoani Dodoma, wamefanya kazi nzuri barabara zote zipo kwenye viwango vizuri hata wakazi wanaoishi jirani na barabara hizi unaona wanavyofurahia barabara hizi", alisema.
Aliongeza kusema kwamba anaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwaajili ya kuboresha miundombinu ya barabara hususani barabara za mijini ambazo zimeleta maendeleo makubwa.
Aidha, akiwa kwenye barababa inayoelekea kiwanda cha mbolea cha Intracom Fertilizer Limited yenye urefu wa Km. 5. Naibu Katibu Mkuu alisema zipo fedha ambazo serikali imeongeza ambazo zinatumika katika maendeleo ya miundombinu ya barabara inayoenda kwenye viwanda ili kurahisisha usafirishaji wa malighafi kutoka nje ya kiwanda.
Hata hivyo, Mhandisi Mativila alisema barabara hiyo inaruhusu magari yenye kubeba mizigo yenye uzito wa Tani 56 na hivyo kurahisisha usafirishaji wa malighafi kutoka nje ya kiwanda na pia mbolea toka kiwandani na kuwafikia wananchi kwaajili ya kilimo.
Naye, Msimamizi wa mradi wa barabara ya Swaswa-Mpamaa yenye urefu wa Km. 8.7 Mhandisi Atuletile Ngailo amesema mradi huo umeweza kuwapunguzia wananchi umbali kwa kutumia barabara hiyo.
Kwa upande wake Meneja wa TARURA wilaya ya Dodoma, Mhandisi Emmanuel Mfinanga alisema barabara zilizojengwa mjini zimekuwa mkombozi kwa wananchi

Comments
Post a Comment