Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali Yawaagiza Wakuu wa Mikoa Kuwakamata Waganga wa Jadi Wanaofanya Ramli Chonganishi



Na Angela Sebastian-Muleba

IKIWA zimepita siku 24 tangu yalilipotokea mauaji ya kikatili kwa mtoto mwenye ualbino marehemu Noela Asimwe Novart ( 2.5) katika kijiji cha Bulamula kata Kamachumu Wilayani Muleba mkoani Kagera, Waziri  wa nchi ofisi ya Waziri mkuu kazi,vijana ajira na watu wenye ulemavu Deogratias Ndejembi amewaagiza wakuu wa mikoa yote hapa nchini kufanya operesheni maalum nchi nzima.

"Nawaagiza wakuu wa mikoa nchi nzima kufanya operesheni maalum ya kuwakamata waganga wa tiba asilia na tiba mbadala wanaojishughulisha na ramli chonganishi wasio na vibali  na kuwafikisha katika vyombo vya sheria,watu wenye ualbino wana haki ya kuishi kama mimi na wewe hivyo ukatili dhidi yao kwasababu ya tamaa havina nafasi "Ndejembi 

Ametoa agizo hilo  wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupiga ukatili kwa watu wenye ualbino uliofanyika katika kata ya Kamachumu Wilayani Muleba mkoani hapa .

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chama cha watu wenye ualbiino Taifa (TASI) Alfred Kapole ameomba  jamii kuwa suala la kuwalinda watu wenye ualibino wasiachiwe jeshi la polisi tu bali kila mmoja kwa nafasi yake aguswe na kuchukizwa na vitendo viovu wanavyofanyiwa ikiwemo mauaji ya kikatili.

Comments