Mbunge wa Viti Maalum Mkoani Mara Mhe.Ghati Zephania Chomete amehudhuria na kuwakilisha Madiwani Mkoani Mkoa Mara kukabidhi zawadi Kwa Mwenyekiti wa UWT Taifa katika Semina ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.
Katika Semina ambayo imefanyika katika ukumbi wa Sub-Marine iliyoko Manispaa ya Kahama, Mhe Ghati aliongoza zoezi la kukabidhi zawadi mbalimbali za upendo zilizotolewa na Waheshimiwa Madiwani wa Kata Wanawake pamoja na Madiwani wa Viti Maalum Mkoa wa Mara kwa ajili ya Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Mary Pius Chatanda.
Zawadi hizo zilizotolewa kwa lengo la kutambua juhudi, ushupavu na umahiri katika usimamizi madhubuti wa Jumuiya ya UWT Taifa.

Comments
Post a Comment