Siku chache baada ya Tanzania kutwaa Tuzo ya Dunia kuwa Sehemu Maridhawa Zaidi kwa Utalii wa Safari Duniani (World’s Leading Safari Destination 2024), Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana amepokea tuzo hiyo rasmi jijini Dodoma.
Waziri Pindi Chana amepokea Tuzo hiyo mbele ya wadau wa utalii na uhifadhi wakiwemo maafisa wanyamapori kutoka wizara 138 nchini wanaohudhuria mafunzo mbalimbali ya utalii na uhifadhi mjini Dodoma na kusema Tuzo hiyo ni matokeo ya kazi kubwa ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na wadau wenyewe wa uhifadhi na utalii.





Comments
Post a Comment