Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amewataka waajiri na viongozi katika ofisi za umma kuwapa fursa Waandishi Waendesha Ofisi (Masekretari) kuwasidia katika uandishi wa Kiswahili sanifu na fasaha katika nyaraka mbalimbali.
Msigwa amesema hayo mkoani Morogoro wakati akifunga Mafunzo ya Matumizi ya Kiswahili Sanifu na Fasaha kwa Waandishi Waendesha Ofisi yaliyosimamiwa na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA).
Amesema, kwa kuwa viongozi na waajiri wengi wana kazi nyingi za kufanya zinazo wafanya wakose muda wa kuandika Kiswahili Sanifu na Fasaha, inabidi wawape fursa Waandishi Waendesha Ofisi wao kwasababu wamepata mafunzo ya namna ya kuandika kiswahili Sanifu na Fasaha.
Aidha, Msigwa amewataka Viongozi kuwapeleka Waandishi Waendesha Ofisi wao katika Mafunzo ya Matumizi ya Kiswahili Sanifu na Fasaha na Mafunzo mengine ya ndani na nje ya nchi ili waweze kuwasaidia vyema kwakuwa ndio wasaidizi wao wa karibu katika uandaaji wa taarifa na nyaraka mbalimbali za kiofisi.







Comments
Post a Comment