Halmashauri ya Wilaya Misungwi yaweka Mikakati ya Kuongeza Ufanisi Kwenye Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo
Wakuu wa vituo vya kutolea huduma za afya na Elimu, watendaji wa kata na wakuu wa idara Halmashauri ya Wilaya Misungwi Mkoani Mwanza wamenufaika na mafunzo yanayolenga kuongeza ufanisi kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Akizungumza wakati wa Mafunzo hayo,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Misungwi Bw. Addo Missama ameeleza kuwa bila ya maadili mema na uwazi katika utendaji wa shughuli za Kiserikali ni vigumu kufikia malengo ya maendeleo endelevu.
Missama amesema kuwa ili kufikia malengo hayo,kila mmoja katika Serikali anapaswa kuwajibika katika kuhakikisha kuwa rasilimali za umma zinatumika kwa njia inayofaa na kwa manufaa ya wananchi wote.
Naye Kamanda wa Takukuru Wilaya ya Misungwi Bi. Elly Makala amesema kuwa kuelekea maadhimisho ya sikukuu ya Maadili tarehe 10/12/2024 kuna umuhimu wa kuimarisha maadili katika utendaji wa majukumu ya kiserikali na jamii ikiwa ni pamoja na kuzingatia kanuni za maadili katika kazi zao ili kujenga imani na uaminifu kutoka kwa wananchi katika kufanikisha ukamilishaji wa miradi ya kimaendeleo.
Bi. Elly amehimiza Kuwepo Kwa Ushirikiano na Uwajibikaji Miongoni mwa Sekta Mbalimbali ikiwemo Elimu na Afya pamoja na kuheshimiwa kwa Haki za Binadamu na Kujiepusha na Rushwa kwenye kila hatua ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo
Afisa Mipango wa Wilaya ya Misungwi Bi. Piniel Titto amesema kuwa Kikao hicho kimelenga pia kujadili mikakati ya kuboresha huduma za afya na elimu ikiwa ni pamoja na kutambua kuwa maendeleo hayawezi kupatikana bila ya ushirikiano wa karibu kati ya Serikali, wananchi na wadau mbalimbali.
Afisa ugavi wa Halmashauri Wilaya ya Misungwi Bw. Andrew Ndaki amewataka Watendaji wa kata,Walimu na Wahudumu wa afya kwa kushirikiana na kamati ya ujenzi na utekelezaji wa miradi ngazi ya serikali za vijiji na vitongoji kuhakikisha wanakuwa makini katika ufatiliaji wa manunuzi na usimamizi wa miradi katika kata zao.
Baadhi ya Wakuu wa vituo vya kutolea huduma za afya na elumu na watendaji wa kata watoa pongezi kwa kupata kikao hicho ambapo kitakua msaada katika kufanya kazi kwa weledi na kuyatekeleza yale yaliotolewa na kuelekezwa kaitika kikao hicho ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanasimamia kwa weledi manunuzi ya yanayohitajika Katika miradi.
Kikao hicho kilidhuriwa na Maafisa Takukuru ngazi ya Wilaya ,Wakuu wa idara Halmashauri ,Wakuu wa vituo vya kutolea huduma za afya na eliminating na watendaji wa kata.




.jpg)




.jpg)

Comments
Post a Comment