Madereva wa bodaboda watakiwa kuvaa kofia ngumu

GEORGE MARATO TV
0


 Na Dawati la Habari Polisi Mwanza

Madereva wa boda boda watakiwa kuvaa kofia ngumu na kufata Sheria za usalama barabarani pindi wanapotumia pikipiki ili kuepukana na ajali ambazo zinaweza wapelekea kupoteza nguvu kazi ya taifa. 

Hayo yamebainishwa Oktoba 24.2024 na Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza  Mrakibu wa Polisi (SP) Sunday Ibrahim wakati akitoa  elimu ya usalama barabarani kwa  waendesha boda boda wa vituo vya kata za Nyegezi, Luchelele na Mkolani wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.

Akizungumza na madereva wa boda boda hao kutoka kanda ya Mwanza kusini,Sunday amesema elimu hiyo  imelenga kuwapa uelewa makundi mengine ya watumiaji wa barabara  hususan bodaboda ili kuzuia ajali zinazoweza kuepukika.

Aidha, SP Sunday amesema, atahakikisha operesheni inayoendelea haimuacha mtu ambapo watakaobaini kutovaa Korea ngumu kinyume cha sheria watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani. 

" wengi mnasema abiria hataki kuvaa kofia ngumu afisa msafirishaji mzuri wa kisasa wa mwanza atampa elimu kabla ya kuondoka juu ya umuhimu wa kofia ngumu" amesema SP Sanduy.

Kwa upande wake mwenyekiti wa  wa waendesha pikipiki wilaya ya Nyamagana Mohamed idi  amewataka waendesha bodaboda hao kuacha kujichukulia sheria mikononi  kwani yeyote anayekosea kuna sheria inatakiwa kumuhukumu hivyo, ni wajibu wa kila mmoja kumlinda mwezake ili kazi hiyo iendelee kuoneka ni njema na ni safi Kwa jamii.

"Kujichukulia sheria mikononi unaweza kupoteza haki yako hivyo tuache mamlaka zifanye kazi zake" amesema Mohamed Idd.

Naye koplo wa Polisi Rehema wa kikosi Cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza amewataka madereva wa bodaboda kuzingatia Sheria za usalama barabarani kwa   kuacha kupakia abiria zaidi ya mmoja katika bodaboda. 

" sheria ya usalama  barabarani inatukumbusha mara zote hasa unapoingia barabarani kwani alietengeneza chombo hiki amekipa uwezo wa kubeba abiria mmoja kwenye hiyo pikipiki maana yake  ni nini anajua pikipiki  hiyo itakapopata shida utapata namna ya kumudu hicho chombo" amesema Cpl Rehema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top