Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu,kazi,ajira,vijana na Wenye ulemavu Ridhiwani Kikwete amewaasa Vijana nchini kuwa mabalozi wa amani na usalama na kushiriki ulinzi wa nchi yao.
Kikwete ametoa wito huo kwa niaba ya Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa wakati akifunga kongamano la kitaifa la Agenda ya Amani na Usalama kwa Vijana lililofanyika Mjini Dar es salaam kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Waziri Kikwete pia amewakumbusha vijana juu ya hatua mbalimbali zinazofanywa na serikali kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo lile la ukosefu wa kazi, athari za matumizi mabaya ya Teknolojia na itandao katika kupashana taarifa muhimu zinazowahusu vijana, Uundwaji wa Baraza la Vijana, Uwezeshwaji na Wenye ulemavu.





Comments
Post a Comment