Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza leo tarehe 22 Septemba 2024, limefanya mazoezi ya utayari kuzunguka maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.
Mazoezi hayo yamefanyika kwa lengo la kujiweka tayari kukabiliana na viashiria na vitendo vya uvunjifu wa amani hususan maandamano haramu yaliyoitishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Akizungumza wakati wa maonyesho hayo ya utayari Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi Wilbrod Mutafungwa amesema Jeshi la Polisi limejipanga kikamilifu kukomesha vitendo hivyo na kuimarisha doria maeneo yote ya Mkoa huo
Chanzo:Dawati la Habari Polisi Mwanza






Comments
Post a Comment