Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh Dr Samia Suluhu Hassan, anatarajia kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya watu wa China mh Xi Jinping yanayolenga kuimarisha uhusiano mzuri na ya kihistoria kwa mataifa haya mawili ulioasisiwa miaka 60 iliyopita.
Rais Samia ambaye ananza ziara ya kikazi nchini China kuanzia Agosti 2 hadi Agosti 06 pamoja na mwenyeji wake Rais wa China,wataungana na Rais Jamhuri ya Zambia Mh Hakainde Hichilema watashiriki na kushuhudia uwekaji saini wa Hati za makubaliano ya uboreshaji wa Reli ya TAZARA.
Rais Samia pia anatarajia kushiriki mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika(Forum on China-Africa Cooperation-FOCAC)utakaofanyika jijini Beijing
Akiwa nchini China Rais Samia atakaohutubia ufunguzi mkutano wa FOCAC kwa niaba ya kanda ya afrika mashariki.