Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikina ma Ubalozi wa Comoro pamoja na TPSF na TANTRADE tunapenda kuwaalika kwenye Ziara ya Kibiashara na Uwekezaji.
Pia wameandaa Kongamano kwa wawekezaji na wafanyabiashara litakalo fanyika tarehe 21 Agosti 2024 katika Ukumbi wa Bunge Jijini Moroni nchini Comoro.
Ziara hiyo italenga Wadau katika Sekta ya Usafirishaji , Kilimo na Ufugaji.
Ukiwa kama mmoja wa wadau wa Sekta tajwa tunaomba tuma taarifa zako ili tuweze kukusajili kwa hatua zaidi ikiwemo kujua gharama zitakazo husika katika Ziara hiyo.
Chanzo: TIC


Comments
Post a Comment