Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Musoma mjini, leo kimemkabidhi fomu ya kugombea nafasi ya Naibu Meya katika halmashauri ya Manispaa ya Musoma diwani wa viti maalum katika halmashauri hiyo Mhe. Naima Minga.
Fomu hiyo ya CCM imetolewa leo Julai 22-2024 na katibu wa CCM Musoma mjini ndugu Barhan Ruta na endapo atapitishwa na vikao vya chama, vitamwezesha Mhe.Naima kushika nafasi hiyo kwa vipindi vitatu mfululizo.
Mhe.Naima ambaye amekuwa mwanachama wa kwanza kuchukua fomu hiyo leo,amekuwa na mvuto mkubwa wa kuendelea kushika nafasi hiyo kutokana na utendaji wake wa kuridhisha hasa baada ya kuwa kiungo kati ya hamashauri na wananchi pamoja na kusimamia vyema utekelezaji wa ilani ya CCM.
Katika tukio hilo pia limeshuhudiwa na katibu wa UWT wilaya ya Musoma mjini Bi Angel Simwanza, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa azimio la UWT la kuwapa nafasi za uongozi wanawake pale wanapojitokeza.
Uchaguzi wa mgombea wa Naibu Meya anayetokana na CCM unatarajiwa kufanyika Julai 26 mwaka huu,kabla ya kuchuana na chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA chenye madiwani wawili kati ya 21 wa CCM.
Halmashauri Manispaa ya Musoma inaongozwa na CCM chini ya mstahiki meya Kapt mstaafu William Gumbo.



Comments
Post a Comment