Aweso: Utendajikazi Uliotukuka Siri ya Rais Samia Kutunukiwa Shahada za Heshima

GEORGE MARATO TV
0


MWANDISHI WETU - DODOMA

Utendajikazi uliotukuka wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa Watanzania na Waafrika kwa ujumla, umetajwa kuwa siri ya kutunukiwa Shahada mbalimbali za Heshima za Udaktari wa Falsafa kutoka vyuo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumzia hayo, Mbunge wa Jimbo la Pangani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amempongeza Rais Dk. Samia kutokana na kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa na uongozi wa Chuo Kikuu cha Nasarawa cha nchini Nigeria Aprili 11, 2026, kwa njia ya mtandao.

"Rais wetu kipenzi Dk. Samia anafanya kazi kubwa za maendeleo, Watanzania, Waafrika na dunia kwa ujumla wanaziona na kuzitambua kazi zake, ndiyo maana amekuwa akitunukiwa Shahada za Heshima. Uongozi wake uliotukuka umekuwa siri ya heshima hizo anazopata," amesema Aweso.

Sanjari na hilo, Aweso amesisitiza kuwa Rais Dk. Samia amejipambanua kwa maneno na kwa vitendo kuwa yeye ni mtekelezaji wa maendeleo ya wananchi ndani na nje ya Tanzania.

Akipokea Shahada hiyo Ikulu, Jijini Dodoma, Rais Dk. Samia amesema "Nilifurahia nilipopokea barua iliyonifahamisha kuhusu Shahada hii ya heshima ambayo imeelezwa kutokana na mchango wangu katika maendeleo bara la Afrika".

Chuo hicho, kimetambua kazi nzuri zinazofanywa na Rais Dk. Samia katika kusukuma ajenda za nishati safi ya kupikia, uwezeshaji wa vijana, uongozi na huduma za afya za mama na mtoto.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top