EWURA NA MISA Tan yaendelea kuwanoa wahariri na waandishi wa habari Nchini

GEORGE MARATO TV
0






Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini Mwa Afrika kwa kushirikiana na Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeendelea kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari ambao ni wanachama wa MISA Tan toka Mikoa mbalimbali.

Takribani waandishi wa habari hamsini (50) wamehudhuria warsha hiyo yenye kulenga kufanya tathimini ya kuwajengea uwezo kwenye kuifahamu EWURA na majukumu yake.


Mafunzo hayo yalifunguliwa na mgeni rasmi Eng. Lorivii Long'idu ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa EWURA alisema kuwa, waandishi wa habari ni daraja la muhimu kwenye kufikisha taarifa sahihi kwa wananchi juu ya haki zao kwenye huduma za nishati na maji.


Naye Mwenyekiti wa Misa Tan Bwana Edwin Soko aliwataka waandishi wa habari kuandika habari za uwajibikaji ili kuwasaidia jamii kujua haki zao.



Naye  Kaimu Meneja  Mawasiliano wa EWURA Bwana Wilfred Mwakalosi alisema kuwa, ni vyema waandishi wa habari wakajikita kwenye kuandika habari zenye kueleza haki za walaji kwa kina ili watambue haki zao za kimsingi.

Mafunzo hayo yalifanyika kwenye hotel ya Sea Shells Jijini Dar es salaam.




Mwisho

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top