RAIS SAMIA ASEMA MAONESHO YA SABASABA NI KIELELEZO CHA TANZANIA KUWA LANGO LA BIASHARA AFRIKA MASHARIKI
Rais Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa maonesho ya Sabasaba ni jukwaa muhimu la biashara na ni ishara muhimu ya uaminifu kwa Tanzania kuwa ni kituo kikuu cha biashara katika lango la Afrika Mashariki.
Akizungumza leo Jijini Dar es salaam, katika maadhimisho ya miaka 50 ya maonesho ya Sabasaba, Rais Samia amesema katika kuadhimisha miaka 50 ya maonesho ni hatua muhimu kwa Tanzania katika kufurahia juhudi za wafanyabiashara, ubinifu wa sekta binafsi pamoja na mchango wa viwanda na nafasi ya Tanzania katika biashara kikanda na kimataifa.
Aidha, Rais Samia, amewataka wadau wa biashara na uwekezaji kujikita katika ubunifu ili kuimarisha maendeleo na ushindani katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba).
Sambamba na hilo, Rais Samia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Dkt. Daniel Chapo, kwa kukubali kuwa mgeni rasmi na kufungua maadhimisho hayo ya miaka 50 ya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam.
Aidha, Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amesema kuwa katika mwaka uliopita mauzo ya bidhaa za Tanzania nje ya nchi yamefikia takribani dola bilioni 17 ambapo ni ongezeko la asilimia 15 kulinganishwa na mwaka uliopita
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu TANTRADE, Bi. Latifa Khamisi amesema kuwa katika kipindi cha miakq 50 jukwaa la maonesho la Sabasaba limefanikiwa kuzalisha fursa zenye thamani takribani Trilioni 129.231 ambapo jumla ya nchini 54 zimeshiriki mara 564 katika kipindi cha miaka 50.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa TANTRADE amesema kuwa katika kipindi cha miaka 50 maonesho yamezalisha ajira 631,900 tangu kuanzishwa kwake ambapo mwaka huu inatarajiwa kutoa ajila zaidi ya 21,000.








Comments
Post a Comment