Akiwasilisha taarifa kuhusu hali ya dawa za kulevya kwa waandishi wa habari leoei 29,2026 jijini Dodoma, Profesa Kabudi amesema mwaka 2025 jumla ya tani 26.36 za mirungi zilikamatwa, ikiwa ni ongezeko la asilimia 42.88 ikilinganishwa na mwaka 2024.
Amesema ongezeko hilo linaonyesha kuimarika kwa ufanisi wa operesheni za ufuatiliaji na udhibiti, hususan katika maeneo ya mipaka na njia zinazotumika kusafirisha dawa hizo nchini.
Kwa upande wa dawa za kulevya za viwandani, Profesa Kabudi amesema Serikali ilikamata kilogramu 907.18 za methamphetamine, kilogramu 672.23 za heroin, kilogramu 4.89 za cocaine, pamoja na gramu 178 za MDMA na gramu 7.82 za MDA.
Aidha, amebainisha kuwa kwa mara ya kwanza mwaka 2025, Serikali ilifanikiwa kukamata tani 29.52 za dawa mpya ya kulevya aina ya Kratom, inayotokana na mmea unaojulikana kama Mitragyna speciosa.
Profesa Kabudi ameongeza kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya kuimarika kwa ushirikiano kati ya vyombo vya dola, taasisi za udhibiti na wadau mbalimbali katika kuimarisha mapambano dhidi ya biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini.







Comments
Post a Comment