Dkt Mwigulu: Tutamuenzi kwa vitendo marehemu Jenista

GEORGE MARATO TV
0




WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itayaendeleza mambo yote yaliyofanywa na mbunge wa Peramiho mkoani Ruvuma, Marehemu Jenista Mhagama kuweka ushiriki kati ya Serikali na taasisi ya kidini.

Amesema marehemu Jenista alikuwa mpatanishi akiunganisha fedha mbalimbali za pamoja na Serikali ambapo hadi leo wanaushirikiano mkubwa, pia aliimarisha umoja na mshikamano kati ya Serikali na sekta binafsi na kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa.

“Marehemu Jenista amekuwa anaamini katika mafanikio na hiyo ndio iliyompa jina la kiraka kwa kuwa kila nafasi aliyopewa aliimudu kwa ukamilifu. Jenista amegusa maisha ya wengi, mimi nilikuwa nashirikiana naye katika masuala ya uongozi na alikuwa mmoja wa marafiki wa familia.”

Ameitoa kauli hiyo leo Jumatatu, Desemba 15, 2025, wakati akiwasilisha salamu za Serikali aliposhiriki Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Jenista Mhagama iliyofanyika katika kanisa Katoliki la Abasia ya Mtakatifu Benedicto, Peramiho.

Katika salamu hizo, Waziri Mkuu amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemuagiza awahakikishie Watanzania wakiwemo Wana-Ruvuma kuwa Serikali itaendelea nao kama ilivyokuwa wakati wa uhai wa Jenista.

“Mheshimiwa Jenista alikuwa kiungo kati ya Wana-Ruvuma na Wana-Peramiho na alikuwa kiungo kati ya Kanisa na Serikali, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amenituma niwahakikishie wote kwamba Serikali itaendelea kuyaenzi mema yote aliyoyafanya enzi za uhai wake.”

Vile vile, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwahakikisha watoto wa marehemu kwamba itakuwa peke yao, wataendelea nao, ambapo amewasisitiza watoto hao waendelee kumtanguliza Mwenyezi Mungu mbele huku wakishikamana na kupenda somo ambalo ambalo amewaachia.

.Kwa upande wake, Spika wa Bunge, Mussa Zungu amewashukuru viongozi wa Serikali na viongozi wa dini kwa kazi kubwa waliyoifanya kutokea kwa msiba.

Awali, Victor Mhagama ambaye ni mtoto wa Marehrmu Jenista ameishukuru Serikali kwa kuendelea wanaoendelea kuutoa kwa tukio kutokea kwa msiba huo huku akiiomba Serikali na wananchi kwa ujumla waendelee kuwa pamoja nao.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top