Rais Samia Kulihutubia Taifa Kupitia Wazee wa Dar es Saalam

GEORGE MARATO TV
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan  anatarajia kuzungumza na wazee wa Dar Es Salaam kesho Desemba 2, 2025 baada ya mikoa huo kuendelea kurejea katika hali yake ya amani.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa huo Albert John Chalamila wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Disemba 01, 2025 ambapo amesema tukio hilo litafanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa JNICC kuanzia saa tano asubuhi.

Ameongeza kuwa Dkt. Samia pia atatumia nafasi hiyo kulihutubia taifa ambapo ataambataana na viongozi wa serikali pamoja na viongozi wasio watumishi wa umma.

“Rais Samia atatumia fursa ya mkutano na wazee hao kulihutubia Taifa,” ni mkutano mwafaka, unaorejesha matumaini na kuendelea kuponya pale ambapo Watanzania waliumia” Amesema Chalamila.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top