Matukio katika Picha.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe Bi *Glory Tausi Shayo,* akiongozana na wagombea Udiwani wa Kata ya Kunduchi, Kata ya Kawe, Kata ya Bunju na, Kata ya Mbezi Juu. Wameendelea na Kampeni za Nyumba kwa Nyumba katika kata ya Kunduchi.
Walifanikiwa kutembelea wafanyabiashara wa Tegeta kwa Ndevu na Kuendelea na Kampeni za Nyumba kwa nyumba, katika mtaa wa Tegeta, Kata ya Kunduchi, Jimbo la Kawe.
Team hii ilipata fursa ya kusikia changamoto nyingi, zinazowakabili wafanyabiashara na wananchi wa eneo hili na wameahidi kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.