Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tuwawezeshe Wafanyakazi Kukabiliana na Mabadiliko ya Teknolojia- Majaliwa

 


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa vyama vya wafanyakazi barani afrika kuweka mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia duniani.

Amesema kwa kufanya hivyo kutawawezesha kupunguza hatari ya kupoteza ajira kutokana na ujio wa mashine pamoja na matumizi ya teknolojia mpya ikiwemo za akili mnemba.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa 22 Agosti 2025,) Alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Afrika (OAUUT) uliofanyika Hoteli ya Johari Rotana Dar es Salaam.

Amesema kuwa, katika dunia ya sasa, imeshuhudiwa uwepo wa mabadiliko makubwa yanayochagizwa na mapinduzi ya kiteknolojia ikiwemo matumizi ya akili mnemba pamoja na utandawazi.

“Kuna hatari ya watu kupoteza ajira zao kadri mitambo na mifumo ya kisasa inavyochukua kazi ambazo kwa kawaida zingeweza kufanywa na wafanyakazi. Tunapaswa kuweka mpango wa kutoa mafunzo endelevu yanayoendana na mabadiliko ya teknolojia ili kuwandaa wafanyakazi na aina mpya za ajira zinazojitokeza.”

Amesema kuwa Tanzania kwa upande wake chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka mikakati ya kukabiliana na mabadiliko hayo ikiwemo kuhamasisha matumizi sahihi ya teknolojia mpya ikiwemo akili mnemba na kusisitiza ulinzi wa haki na faragha za wafanyakazi. “Teknolojia lazima ilinde utu na si kudhoofisha heshima ya kazi.”

Amesema eneo lingine ni kuwajengea uwezo wafanyakazi kupitia programu mbalimbali zitakazowawezesha kuwaongezea ujuzi katika kazi. “Tunafanya hivi ili kuhakikisha watu wetu hasa vijana wanajengewa maarifa na stadi zinazohitajika hasa katika maeneo ya  uchumi wa kijani na kidijitali.”

Aidha, amesema Serikali inathamini na kutambua mchango mkubwa wa vyama vya wafanyakazi nchini na itaendelea kushirikiana nao katika kuboresha masilahi ya wafanyakazi.

"Serikali imevipa nafasi vyama vya wafanyakazi kufanya kazi kwa Uhuru na bila kuingiliwa tunawasihi kuendelea kushauriana na kushirikiana na Serikali ili kuendelea kuboresha maslahi na mazingira ya ufanyaji kazi."

Amesema ushirikiano mzuri uliopo baina ya Serikali na vyama hivyo umeiwezesha Serikali kutekeleza mahitaji yote muhimu ya wafanyakazi nchini, ikiwemo maboresho ya Sera, Sheria na maslahi ya wafanyakazi.

Kadhalika, amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kuunga mkono jitihada za Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Afrika (OAUUT) ikiwa ni sehemu ya kuenzi jitihada za Baba wa Taifa ambae ni mwanzilishi wa Shirikisho hilo.

Naye Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, amesema Serikali imeendelea kushirikiana na vyama vya wafanyakazi nchini na imepitisha Sera na Sheria mbalimbali katika kuhakikisha inarekebisha na kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

Kwa Upande wake, Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Afrika (OATUU), Joshua Ansah amesema  chama hicho kitaendelea kusimamia na kuhakikisha kinasimamia maslahi ya wafanyakazi Barani Afrika, ili kuhakikisha usawa na maslahi kwa wafanyakazi wote.

Aidha, ameshukuru viongozi wa vyama vya Wafanyakazi Afrika kwa kuendelea kuunga Mkono Shirikisho hilo katika kufanikisha jitihada za kupigania maslahi ya wafanyakazi.

"Tuendelee kuunga mkono Shirikisho letu kwa Maslahi mapana ya wafanyakazi barani Afrika na pamoja tutaendelea kusimamia na kupigania kuboresha maslahi yao."

Naye, Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la wafanyakazi Kanda ya Afrika Mashariki (ILO) Bi. Caroline Mugala, Amesema Chama hicho kitaendelea kusimamia umadhubuti na ufanisi wa vyama vya wafanyakazi ili kuhakikisha Serikali zinaendelea kusimamia maslahi ya wafanyakazi.

"Tunahitaji kuendelea kuwalinda wafanyakazi wetu kutokana na mabadiliko mbalimbali ya kijamii ikiwemo mazingira na teknolojia ni muhimu wafanyakazi waendelee kupewa mafunzo na kuwezeshwa kukabiliana na mabadiriko haya."

Amesema ni lazima kila mabadiriko yanayowahusu wafanyakazi yawahusishe wafanyakazi hao na wakubaliane nayo ili kuwa na manufaa kwa pande zote mbili.

Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Vyama vya  Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Nyamhokya, amesema chama hicho kinajivunia mafanikio makubwa ambayo kimeyapata kwa kupigania haki za wafanyakazi wote Nchini.

Amesema mafanikio hayo yametokana na mahusiano mazuri ambayo chama hicho kimeyajenga na Serikali pamoja na watumishi jambo ambalo limewezesha chama hicho kufikia malengo yake na kufanya kazi kwa ufanisi

"Tumetumia kwa kiasi kikubwa njia ya majadiliano na maridhiano katika kufanikish mahitaji ya wafanyakazi tunashukuru kwa Upande wetu Serikali yetu imekuwa sikuvu kusikiliza na kutatua changamoto zinazo wakuta wafanyakazi.

Amesema chama hicho kimefurahia kuwa sehemu ya mafanikio na kuhost mkutano Mkuu wa vyama vya wafanyakazi Afrika.

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi wa Afrika OATUU lilianzishwa mwaka Aprili 1973 na Rais wa Kwanza wa Tanzania Julius Kambarage Nyerere na Rais wa kwanza wa Ghana Fransis Kwame Nkuruma kwa lengo la kuwaunganisha wafanyakazi na kusimamia maslahi ya wafanyakazi Barani Afrika kwa pamoja.




Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...