Na Ada Ouko, Bunda.
MKOA wa Mara unatarajia kukimbiza Mwenge wa uhuru takriban kilometa 1123 katika wilaya sita na Halmshauri tisa za mkoa huo, sambamba na kuweka mawe ya msingi kuzindua na kufungua miradi 68 ya maendeleo ya wananchi yenye thamani ya shilingi Bilioni 26.5
Hayo yamebainishwa Agosti 15,2025 na Katibu tawala wa Mkoa huo Gerald Kusaya wakati akipokea Mwenge huo kutoka kwa Katibu tawala wa mkoa wa Simiyu Prisca Kayombo, Makabidhiano hayo yamefanyika wilayani Bunda mkoani humo.
"Mkoa wa Mara umejipanga kushiriki mbio za Mwenge wa uhuru kikamilifu ambapo katika mbio hizo utatembea kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maendeleo ya wananchi 68 . yenye thamani ya shilingi 26.5 ambapo miongoni mwa miradi hiyo ni sekta za Afya,Maji, Elimu, Ujenzi,Kilimo, Mifugo, Mazingira, Ustawi wa jamii, Viwanda na Biashara" alisema Gerald.
Aidha amesema Mwenge huo ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julias Nyerere utakapopita wilaya ya Butiama utapata nafasi ya kuwasha mwenge wa Mwitongo nyumbani kwa Mwl. Nyerere, ambapo viongozi wa mbio za Mwenge kitaifa watazuru kaburi la Hayati Nyerere na kuweka shada la maua pamoja na kutembelea makumbusho.
Amesema mbio za Mwenge huo mwaka huu 2025 umelenga kuwaelimisha, na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu wa chini ya kauli mbiu isemayo "jitokeze kushiriki uchaguzi mkuu mwaka 2025 kwa amani na utulivu" uchaguzi huo utakaofanyika ifikapo October 29,2025.
Kusaya amesema ifikapo kipindi hicho Taifa litakuwa na jukumu kubwa la kikatiba na kidemokrasia la uchaguzi wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani katika kuleta maendeleo ya wananchi, ambapo amewataka wananchi wenye sifa kikatiba wajitokeze kwa wingi kushiriki uchaguzi huo.
Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ismaily Ally amehaidi mkoa huo kukimbiza Mwenge wa uhuru katikati hali ya usalama, kuonyesha amani, upendo na ushirikiano wa hali ya juu kwa viongozi watendaji wa Halmashauri zote tisa na wilaya sita Mkoani humo , Mbio hizo za mwenge zitahitimishwa October 23 , 2025.