Azania Bank Kinara Sabasaba 2025,Yashinda Tuzo Mbili

GEORGE MARATO TV
0

 

Azania Bank imeibuka kidedea kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya maonesho hayo ya kimataifa jijini Dsm.

Azania Bank imetwaa tuzo ya mshindi wa kwanza ya muoneshaji bora kwenye sekta ya fedha ikizishinda benki zote zilizoshiriki maonesho hayo kwa mwaka huu. Pia imeibuka mshindi wa pili wa jumla katika waoneshaji wote.

Tuzo za washindi zilikabidhiwa na Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi aliyekuwa mgeni rasmi siku ya ufunguzi.

Akizungumza katika maonesho hayo wakati Mh. Rais wa Zanzibar alipotembelea banda la Benki hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa Azania Bank Bi. Esther Mang’enya alisema kuwa kwa mwaka huu walijikita katika kutoa huduma za kidijitali na kuonesha ni jinsi gani zinaleta tija kwa mfanyabiashara sambamba na kauli mbiu ndogo ya maonesho ya Sabasaba mwaka huu inayosema ‘’Sabasaba 2025,Kidijitali zaidi’’.

Itakumbukwa kuwa mwanzoni mwa mwaka huu Azania Bank ilizindua toleo jipya la huduma zake za kidijitali la Azania Digital linalobeba huduma zake kama za Whatsapp Banking, Internet Banking, Azania Wakala,Mobile Banking nk. zilizoboreshwa zaidi.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top