Mkuu wa Kikosi Ffu Mara Ahamasisha Wadau Kuandaa Matukio ya Michezo

GEORGE MARATO TV
0


Na Shomari Binda-Musoma 

MKUU wa Kikosi cha Kuzuia na Kutuliza Ghasia ( FFU) mkoani Mara ASP Edwin Mwaisanila amewaita wadau wa michezo kujitokeza kuandaa mashindano mbalimbali.

Wito huo ameutoa leo juni 2,2025 kwenye uwanja wa Kamnyonge shule ya msingi kwenye mchezo wa kirafiki kati ya FFU Mara na Buhare fc.

Mchezo huo ulikuwa maalum kuikabidhi cheti cha ushindi timu ya FFU Mara baada ya kuibuka washindi kwenye bonanza la miaka 61 ya Muungano.

Akizungumza uwanjani hapo Mwaisanila amesema  Musoma na mkoa wa Mara kuna vipaji vikubwa na vinapaswa kuendelezwa.

Amesema kuendelezwa kwa vipaji hivyo ni kuandaliwa kwa mashindano mbalimbali yakiwemo mabonanza.

Mkuu huyo wa FFU Mara amesema viongozi wa michezo wanapaswa kuwa karibu na wadau na kuwashawishi kuandaa michezo hiyo.

" Musoma na mkoa wa Mara kuna vipaji vikuɓwa vya michezo ambavyo vinapaswa kuendelezwa ili baadae wanufaike kiuchumi kupitia michezo.

" Kuendelezwa ni pamoja na kuanzishwa kwa michezo na mabonanza mbalimbali kama ambavyo yanafanyika maeneo mengine",amesema.

Katika mchezo huo wa kirafiki tomu ya FFU Mara wamechomoza na ushi ndi wa bao 1-0 dhidi ya Buhare fc kwenye mchezo uliokuwa na ushindani kwa dakika zote za mchezo.












Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top