Wabunge Tanga watuma salamu kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan*

GEORGE MARATO TV
0

 


📍 Wazipitisha kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar 

📍 Wasema Tanga ipo salama, wasubiri uchaguzi ufike wampe kura za mafuriko

Na wandishi Wetu, Tanga 

WABUNGE wa mkoa wa Tanga, wamempa salamu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zubeir Ali Maulid afikishe salamu kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwamba majimbo yote 15 ya mkoa huo yatakuwa na wabunge wa CCM.

Aidha, wabunge hao pia wamesema wanasubiri uchaguzi ufike mwezi Oktoba mwaka huu ili wananchi wa Tanga waongoze kwa kumpa kura nyingi Rais Dkt Samia.

Akizungumza kwa niaba ya wabunge hao kwenye uwekaji jiwe la msingi jengo la soko la Machinga Jijini Tanga, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na mbunge wa Mkinga, Dastan Kitandula alimuomba spika huyo apeleke salamu kwa Rais kwamba mkoa huo kupitia wabunge hao umejipanga kuendelea kuifanya Tanga kuwa ya kijani.

Alisema wanamshukuru Rais kwa kazi kubwa aliyoifanya katika mkoa huo kwa kuipatia miradi ya maendeleo karibu kila kijiji hatua ambayo imeleta tija kwa wananchi.

"Mheshimiwa spika Mimi ni Mwenyekiti wa wabunge wa mkoa wa Tanga, naomba utupelekee salamu kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwamba majimbo yote ya Tanga CCM itashinda, lakini pia kwa niaba ya wananchi wetu shukrani zetu kwake ni kumpa kura nyingi kuliko mkoa mwingine wowote ule kutokana na kazi alizofanya," alisema Kitandula.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu (MCC) Rajabu Abdallah alisema kuwa mkoa wa Tanga unaendelea kumshukuru Rais kutokana na miradi ambayo ametekeleza katika mkoa huo.

Alisema kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Rais mkoa huo unajipanga ili kuhakikisha wanashika nafasi ya kwanza kwa kumpa kura nyingi katika uchaguzi huo.

Akizungumza kuhusu soko hilo la Machinga Mwenyekiti alimshukuru Rais kwa kurasimisha kazi za vijana wanaotembeza nguo mikononi na kuwajengea maeneo maalum ili waweze kuuza na kujiendelesa kiuchumi.

"Soko hili likikamilika litakuwa ni la kisasa sana na litakuwa ni eneo lenye thamani kubwa hivyo ni vema vijana wakalitumia kujijenga kiuchumi kama makusudio ya serikali", alisema.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batlida Salha Burian alisema mkoa huo umepata miradi mingi ya kimkakati ikiwemo upanuzi wa bandari ya Tanga ambayo Sasa kwa mwezi meli 34-35 zimekuwa zikitia nanga na vijana kupata ajira.

"Tunaomba utufikishie salamu kwa Rais kuhusu ziara yako hii matumaino yetu kwake na namna tulivyojipanga kumpa kura nyingi, lakini pia umetupa elimu ya Muungano," alisema.

Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi jengo la Machinga Spika alisema kuwa Watanzania lazima tuulinde Muungano kwakuwa umekuwa ni wa kidugu.

Alisema nchi mbalimbali zikiwemo za Senegal na Gambia zilitaka kuiga Muungano kama wa Tanganyika na Zanzibar lakini wameshindwa hivyo ni lazima vijana wa Sasa tuulinde na kuudumisha Muungano huo.

Alisema Muungano huo umekuwa na mahusiano ya karibu kwa watu kutoka pande zote za Muungano kufanya shughuli za kiuchumi bila bughuza ikiwemo kuoleana.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top