Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kusingi Unguja, Mhe. Wanu Hafidh Ameir amefungua mafunzo elekezi kwa viongozi na watendaji wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kuanzia ngazi ya Matawi, Wadi, Jimbo na Wilaya yaliyofanyika kwenye ukumbi wa TASAF, Zanzibar
Wanu amefungua mafunzo hayo tarehe 20 Aprili, 2025 yenye lengo la kuwajengea uwezo viongozi na watendaji wa UWT hasa kutokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapoelekea kushiriki uchaguzi mkuu wa kuchagua Rais, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani nchi nzima ifikapo mwezi Oktoba, 2025.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Mhe. Wanu Ameir amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha viongozi hao wa UWT ngazi zote kukumbuka wajibu wao hasa CCM inapokuwa kwenye uchaguzi na kupanga mipango ya ushindi
Mhe. Wanu Ameir amewasisitiza wanawake kuwa wasisite kujitokeza kuchukua fomu na kugombea nafasi za uongozi wa dola nchini kwani Wanawake wanaweza lakini ni lazima kwanza wathubutu kwa kuonesha nia ya kuwatumikia wananchi
Mwisho, Mhe. Wanu Ameir amewapongeza viongozi na watendaji wote wa UWT kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki mafunzo hayo kwani hii imeonyesha wazi kuwa UWT wako tayari kujifunza ili kuongeza ufanisi katika majukumu yao.