Na Angela Sebastian; Biharamulo.
Watu wawili wa familia moja wamefariki dunia huku Wahisiwa 44 wakiendelea kuwekwa chini ya ungalizi wa wataalam wa Afya wakiwa majumbani kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa marburg uliotokeaWilayani Biharamulo mkoani Kagera.
Watu 281 walihisiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya marburg ambapo 145 kati ya hao waliwekwa chini ya uangalizi katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma baada ya kusambaa kwa ugonjwa huo.
Kutokana na taarifa ya Wizara ya Afya watu hao 145 waliokuwa chini ya uangalizi kwasasa wameruhusiwa kuungana na familia zao baada ya wataalam wa afya kujiridhisha kuwa hawana maambikizi ya virusi hivyo.
Naibu waziri wizara ya Afya Dk.Godwini Mollel amefanya ziara ya kutembelea Kambi za wahisiwa wa virusi vya Marburg katika Wilaya ya Biharamulo na kupata taarifa juu ya mwenendo wa ugonjwa huo kwasasa kutoka kwa Mkurugenzi wa huduma za kinga wizara ya Afya Ntuli Kapologwe.
Amesema wahisiwa 92 wanaendelea na uangalizi katika kambi mbalinbali za kutolea huduma za Afya kwa kufanya uchunguzi mbalimbali na kujua hali zao zinaendeleaje ndani ya siku ya siku 21.
Amesema mpaka sasa kwa kushirikiana na Mashirika ya kimataifa na Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii tayari Kaya 10,892 wamepatiwa Elimu ya kujikinga huku vitu o vya ukaguzi wa abiria wanaotoka nchi mbalimbali vikiongezeka kutoka vituo 8 Hadi 11 ambapo kwa siku abria 8,000 hadi 10,000 wanapimwa hali zao.
Mollel ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kwa kufuata Sheria zinazotolewa na Wizara ya Afya ili kuendelea kukinga afya zao bila kuathiri uchumi wao.
"Nawapongeza wataalam wetu kwa kuchukua hatua za haraka mlizofanya na mnaendelea kutoa huduma katika jamii , ugonjwa huu ni hatari na wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari , kwa kuwa hatua za kujikinga ziko wazi basi wanaweza kuendelea na shughuli zao huku wakijikinga"alisema
Kwa upande wa mkurugenzi wa kinga toka Wizara ya Afya Dk.Ntuli Kapologwe aliyataja mashirika ya kimataifa yanayoendelea kutoa huduma kwa huko Biharamulo kuwa ni WHO,UNICEF na CDC ambao wanaendelea kisaidia Serikali katika mapambano ya ugonjwa huo mpaka sasa.






