Bashungwa Kuzindua Mikakati ya Mawasiliano ya Wizara ya Mambo ya Ndani na Vyombo vyake Vya Usalama

GEORGE MARATO TV
0


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amewasili Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Msalato Dodoma ambapo atazindua Mikakati 6 ya Mawasiliano ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Vyombo vya Usalama ambavyo Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), leo tarehe 09 Januari 2025.

Aidha, Bashungwa atafungua Kikao Kazi cha Mwaka, cha Wasemaji wa Vyombo vya Usalama vya Wizara yaani Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

Hafla hiyo imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally Gugu, Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Maduhu Kazi na Wakuu wa Vyombo vya Usalama na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top