Akizungumza baada ya kutembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa eneo la Mwitongo, kijijini Butiama,Mwanasheria huyo mkuu wa serikali,amesema kufika eneo hilo ni darasa tosha la kufahamu vema historia ya nchi na Baba wa Taifa wa Taifa.
"Tumeona nyumba aliyojengewa na jeshi la wananchi,tumeona vitu vingi vya kujifunza kuhusu Mwl Nyerere pia tumefika kwenye kaburi na kumwombea dua,nawaasa watanzania wengine wakipata nafasi kufika Mara, wafike Butiama ili kupata maelezo ya kazi zake alizowahi kuzifanya wakati wa uhui wake" alisema Mh Hamza Johari.
Hata hivyo Mwanasheria mkuu wa serikali, amepata nafasi ya kupanda juu ya jiwe ulipo Mwenge wa Mwitongo ambao umeasisiwa na Baba wa taifa na kila mwaka wakati wa mbio za mwenge wa uhuru umekuwa ukifika na kuwasha mwenge huo.
Akiwa eneo la Mwitongo Mwanasheria huyo mkuu wa Serikali ametembelea eneo ulipo mwenge wa Mwitongo,ameona sanamu ya Baba wa Taifa,kisha kutoa heshima katika kaburi la Baba wa Taifa na kupata nafasi ya kutembelea maeneo mbalimbali kabla ya kukutana na mtoto wa sita wa Mwl Nyerere Madaraka Nyerere.