Fresha Kinasa-Mara.
Maofisa wa Polisi Dawati laJinsia na Watoto Walipongeza Shirika la Hope for Girls and women in Tanzania kupambana na Ukatili Mara.
Zaidi ya Maofisa wa Polisi 200 kutoka Mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani wanaohusika na Dawati la Jinsia na Watoto wametembelea kituo cha Nyumba Salama kiabakari' kilichopo Wilaya ya Butima Kinachotoa hifadhi kwa Wasichana waliokimbia vitendo vya Ukatili ukiwemo ukeketaji kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mara.
Maofisa hao wametembelea kituoni hapo Dicemba 11, 2024 Ambapo wakiwa katika kituo hicho ambacho kinamilikiwa na Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania, (HGWT) wamepongeza kazi zinazofanywa na Shirika hilo ikiwemo kuwapa hifadhi Wasichana hao, elimu ya ukatili, haki zao na msaada wa kisaikolojia.
Pia, hatua ya Shirika hilo katika kuwaendeleza kifani na kitaaluma, pamoja na juhudi za utoaji wa elimu ya ukatili kwa Jamii ili kutokomeza vitendo hivyo ambavyo ni kinyume cha sheria za nchi na haki za binadamu.
Akizungumza na Wasichana hao Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi kutoka Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es laam (SSP) Anitha Semwano amewapongeza Wasichana hao kwa uamzi wa kukimbia ukeketaji kutoka katika familia zao na kwenda kupata hifadhi katika kituo hicho. Huku pia akiwaomba kujitambua na kutumia vyema fursa ya kuwa kituoni hapo kwa manufaa yao ya baadaye.
"Nafurahi kuwaona Watoto mna furaha kubwa mkipata hifadhi hapa, pia napongeza huduma nzuri mnazopata hapa ikiwemo malezi bora kutoka kwa Mkurugenzi Rhobi Samwelly. Hakika anafanya kazi kubwa licha ya kuwa na watoto wengi amewajenga kujiamini na kuishi kwa upendo."amesema.
Pia, ametoa wito kwa Jamii kushiriki kikamilifu kuwalinda Watoto wa kike dhidi ya ukeketaji na aina mbalimbali za ukatili. Huku akihimiza mila mbalimbali zenye madhara ziachwe kwa sababu hazina faida.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika hilo Rhobi Samwelly amelipongeza Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto Mkoani humo kwani wameendelea kufanya kazi kwa karibu na kwa ushirikiano ikiwemo kutoa elimu ya ukatili wa Kijinsia katika Jamii na kuwaokoa Wasichana katika hatari ya kukeketwa.
Aidha, Rhobi ameongeza kuwa kuanzia Dicemba Mosi, 2024, hadi Dicemba 10, 2024, wasichana 246, wamepokelewa na Shirika hilo katika vituo vyake vinavyotoa hifadhi kutoka katika familia zao baada ya kukimbia ukeketaji.
Ambapo, kituo cha Hope Mugumu Nyumba Salama wasichana 45, kituo cha Nyumba Salama kiabakari wasichana 189 na msimu huu ni wa ukeketaji ambapo Koo nyingi zinakeketa na ameiomba Watoto wa kike wasomeshwe na kuwezeshwa kusudi watimize ndoto zao.
Rhobi Mwita ambaye ni mmoja wa Wasichana wanaopata hifadhi katika kituo hicho amewaomba Maofisa hao wa Polisi, kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi katika kushughulikia ulinzi na usalama wa mtoto kwani dhamana hiyo wamepewa na Mwenyezi Mungu.
Maofisa hao, wamepata fursa ya kusikiliza shuhuda mbalimbali kutoka kwa wasichana hao waliokimbia ukeketaji na kula nao chakula cha pamoja.