Wafanyabiashara soko la kimataifa la mwaloni kirumba walia na hatua ya sehemu ya soko hilo kugeuzwa bandari

GEORGE MARATO TV
0



 Siku chache baada ya Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania(TPA)kuanza kusimamia utendaji kazi wa kibandari katika mwalo wa kirumba manispaa ya ilemela Jijini Mwanza,wafanyabiashara wa soko la kimataifa la mwaloni kirumba wamepinga uamuzi huo.

Wafanyabiashara hao wanadai kuwa hatua ya Tpa kuchukua usukani wa shughuli za kibandari katika eneo hilo imeanza kuathiri shughuli zao zikiwemo za usafirishaji.



Wakizungumza na waandishi wa habari,baadhi ya watoa huduma za usafirishaji katika eneo hilo wameiomba serikali kupitia upya uamuzi wake ili kuongeza ufanisi kwenye uendeshaji wa shughuli zao.

Wamedai kuwa kabla Mamlaka ya usimamizi wa bandari kuanza kusimamia utendaji kazi wa mwalo wa kirumba,mitumbwi inayosafirisha abiria iliruhusiwa kubeba mizigo kidogo tofautina sasa.




‘’Tokea bandari waingie eneo hili,mitumbwi ya abiria hairuhusiwi kubeba mzigo wowote,hili linatuathiri na hatupati faida kutokana na abiria kupatikana wakati wa giza ikilinganishwa na wakati wa mbalamwezi’’alisema Fatuma Kasenda Mmoja wa wasafirishaji kwenye mwalo wa kirumba

Naye Mwenyekiti wa soko la kimataifa la samaki la mwaloni kirumba Fikiri Magafu ameomba kuondolewa kwa muda wa ukomo wa usafirishaji kwenye ziwa victoria wa saa 12 za Jioni kutokana na sheria hiyo kuchangia wasafirishaji kwenye ziwa victoria kutoa huduma hiyo kwa hasara.

‘’Hili ziwa haturuhusiwi kusafiri usiku,saa zingine ziwa linachafuka na kushindwa kutoa huduma kwa muda muafaka,tuombe serikali ipitie upya sheria hiyo ili kuwezesha wasafirishaji kufanya kazi bila shida’’alisema Magafu

Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tpa ilianza kusimamia shughuli za bandari kwenye mwalo wa kirumba oktoba 12 mwaka huu ambapo Meneja wa bandari kanda ya ziwa victoria Erasto Lugenge amesema kuwa mamlaka hiyo imechukua hatua hiyo ikiwa ni utekelezaji wa tangazo la serikali namba 855 la tarehe 24/12/2023

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza,Lugenge ametaja baadhi ya shughuli zitakazopewa kipaumbele na Tpa kuwa ni pamoja na kudhibiti shughuli za usalama wa vyombo vyote vya majini vinavyoegesha kwenye mwalo huo ili kuhakikisha kuwa abiria na mizigo inayosafirishwa inakuwa salama.

Mipango ya baadaye ya mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania ni kujenga miundombinu ya kisasa pamoja na kusimamia  shughuli za upakuaji na upakiaji wa shehena katika mwalo huo pamoja na mialo mingine iliyorasimishwa kupitia tangazo hilo.

“Napenda kuchukua fursa hii kuutarifu umma hususani ni wakazi wa mji wa mwanza pamoja na mikoa Jirani ambao wanatumia ziwa victoria kwamba kuanzia 12/10/2024,Tpa imeanza rasmi utekelezaji wa tangazo hilo la serikali linaloitaka Mamlaka hiyo kusimamia rasmi shughuli za utendaji kazi wa kibandari kwenye mwalo wa mwaloni kirumba”alisema Lugenge na kuongeza kuwa

‘’Faida kubwa ni kuwa sasa vyombo vinavyotoa huduma ya usafiri na usafirishaji vitakuwa vinadhibitiwa rasmi ambapo usalama wa vyombo hivyo utakuwa wa uhakika na tutakuwa tunafahamu abiria wanaondoka na chombo gani na chombo hicho kiko salama au la”

Aidha Meneja Lugenge amewaasa watumiaji wa bandari za ziwa victoria kutumia bandari rasmi kutokana na bandari hizo kuwa na miundombinu kwa ajili ya kutoa huduma huku suala la usalama wa abiria na mali zao linapewa kipaumbele kwenye bandari hizo ikilinganishwa na bandari bubu.

Ziwa victoria upande wa nchini Tanzania lina bandari 358 ambapo kumi ikiwemo mwalo wa kirumba tayari zimerasimishwa huku bandari 348 zilizosalia zikiwa hazijarasimishwa na hivyo kuchangia katika kuhatarisha usalama wa abiria na mali zao pamoja na kutumiwa na wahalifu kupitiza bidhaa haramu sanjari na bandari bubu kutumiwa na baadhi ya wafanyabiashara kukwepa kodi.














Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top