Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro leo Agosti 13, 2024 umempokea Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mhandisi Hamad Masauni.
Mh Masauni ambaye amembelea Ubalozi huo kisha kupata nafasi ya kusalimiana na watumishi ubalozini hapo.
Akiwa katika ubalozi huo waziri huyo wa mambo ya ndani ya nchi, amepokea pia taarifa ya kituo na masuala ya Watanzania waishio Comoro.
Mheshimiwa Waziri Masauni amepongeza juhudi zinazoendelezwa na Ubalozi katika kukuza mahusiano baina ya nchi hizo mbili.






.jpg)
Comments
Post a Comment