Serikali imedhamiria kuimarisha kilimo na ufugaji katika Jeshi la Magereza ili kuliwezesha jeshi hilo kutumia maeneo inayomiliki kwa kilimo chenye tija huku ikiweka wazi nia ya kukutanisha wizara tatu ikiwemo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Kilimo,Mifugo na Uvuvi ili kuweza kuboresha kilimo katika Jeshi la Magereza.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi wakati wa Kikao na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Magereza,kilichofanyika leo Makao Makuu ya Shirika hilo,jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohamed Mahmoud amempongeza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza ambapo pia aligusia kuongezeka kwa mapato kutoka Bilioni 15/= mpaka Bilioni 24/= ambapo mapato hayo yametokana na miradi mbalimbali ikiwemo ya Ujenzi wa Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU),Uzalishaji wa Sabuni,Maziwa,Viatu,Mikoba ambazo bidhaa hizo hutengenezwa kwenye viwanda vilivyopo chini ya Shirika hilo.



