Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Mhe. Agness Marwa, amewatembelea wajasiriamali wa Soko la Free Park, Manispaa ya Musoma, na kujionea shughuli zao za kila siku.
Mbali na kuungana nao katika shughuli za biashara ya dagaa, Mhe. Marwa amewataka kina mama kuendelea kuzungumza na watoto wao kuhusu umuhimu wa kudumisha amani na kuepuka kujihusisha na vitendo vinavyoweza kuvunja utulivu wa nchi, ikiwemo kuitikia wito wa maandamano au vurugu.
Aidha, amewahimiza wajasiriamali hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kujiongezea kipato na kuchangia maendeleo ya familia na taifa.
Kwa upande wao, wajasiriamali wa soko hilo wamesema wamefarijika na ziara ya Mbunge huyo, wakieleza kuwa amekuwa karibu nao mara kwa mara na anaelewa changamoto zao. Pia wamemtakia mafanikio katika majukumu yake ya uongozi.

Comments
Post a Comment