Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian amewataka wananchi wanaoanzisha kampuni binafsi kusajili ndani ya mkoa ili kuongeza mapato ya mkoa Kwa mafunufaa ya mkoa na taifa Kwa ujumla .
Hayo ameyasema alipokuwa akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika katika uwanja wa usagara baada ya matembezi ya furaha ikiwa ni muendelezo wa shughuli maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya mapato Tanzania TRA yaliyoanza tangu tarehe 22 Juni mwaka huu na kilele chake ni tarehe 1 julai mwaka huu.
Aidha Batilda alisema kuwa kufanya hivyo serikali ya mkoa itafikia malengo inayojiwekea Kila mwaka kwani mkoa wa Tanga una fursa nyingi ya kujipatia Kodi ikiwemo bandari,uvuvi,madini pamoja na mipakani.
Sambamba na hayo aliwataka wafanya biashara wote kuweza kutoa risiti na Kwa wale ambao wanapunguza gharama kwenye risiti waache mara moja tabia ya kuiibia serikali hivyo wafanya biashara hususanabwafanya biashara wa madini kuwa makini katika kuangalia risiti kiwango wanachoandikiwa iwe ni ya halali .
Kwa Upande wake Meneja wa TRA Castrol John alisema kuwa TRA ilianzishwa julai 1mwaka 1996 ambapo walikuwa wanakusanya sh.Bilioni 531 Kwa mwaka mpaka kufikia 25-26 trillion 32,hiyo yote imechagizwa na maendeleo ya ukuaji teknolojia.
Aliongeza kuwa ongezeko la mapato hayo pia imesababishwa na usimamizi madhubuti katika ukusanyaji Kodi na elimu Kwa mlipa Kodi iliyokuwa ikitolewa na Kwa walipa kodi pamoja na uhusiano mzuri kati ya TRA na taasisi nyingine.
Aidha Castrol alimalizia Kwa kusema kuwa matarajio Yao ni kuendelea kuhamasisha ulipaji Kodi wa hiyari sambamba na kuboresha teknolojia ya ukusanyaji Kodi.







Comments
Post a Comment