Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeongeza safari maalum ya treni ya umeme ya Mchongoko (EMU) kati ya Dodoma na Dar es Salaam kufuatia kuongezeka kwa idadi ya wasafiri wanaohitaji huduma hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa TRC, Fredy Mwanjala,leo Jun 12,2026 Jijini Dar es salaam, amesema treni hiyo ya ziada itaondoka katika Stesheni ya Dodoma kuelekea Dar es Salaam saa 1:00 usiku leo Ijumaa, Juni 12, 2026.
Amesema uamuzi wa kuongeza safari hiyo umetokana na ongezeko kubwa la mahitaji ya usafiri kwenye njia hiyo, huku TRC ikiendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, salama na yenye uhakika.
Mwanjala amewahimiza wasafiri kukata tiketi mapema kupitia mfumo rasmi wa ukataji tiketi wa shirika hilo ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na ongezeko la mahitaji ya usafiri.
Hatua hiyo inaendelea kuimarisha huduma za usafiri wa reli ya kisasa nchini, huku TRC ikijitahidi kukidhi mahitaji ya wananchi wanaotumia usafiri huo unaozidi kupata umaarufu kila siku.

Comments
Post a Comment