Na beda msimbe,TBN, Moscow.
Urusi imesema taifa hilo litafungua fursa lukuki kwa taifa la Tanzania kwa manufaa ya pande zote mbili.
Aidha taifa hilo lenye miradi 70 yenye thamani ya dola za Marekani milioni434.22 ikiwa imewezesha ajira 3018 tanzania limesema kuwa litatangaza fursa hizo katika mkutano wa uchumi wa kimataifa kesho kutwa.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao chake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kiongozi wa Urusi Vladimir Putin amesema Urusi imekuwa ikifuatilia kwa makini mageuzi yanayofanyika nchini tanzania na wanaona inavyokua.
Amesema amekuwa na mazungumzo yenye manufaa makubwa kwa jamii ya pande zote mbili na kuahidi kuendelea na ushirikiano na Tanzania. Naye rais Samia amesema kuwa ziara yake katika Shirikisho la Urusi ina umuhimu mkubwa wa kihistoria kwake binafsi na kwa taifa la Tanzania kwa ujumla.
“Ziara yangu ina umuhimu wa pekee wa kihistoria kwangu binafsi na kwa nchi yangu. Imepita zaidi ya nusu karne tangu kufanyika kwa ziara ya mwisho ya kiserikali ya Tanzania nchini Urusi. Hivyo, kwangu hii ni safari ya kihistoria sana kuja Urusi kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wa pande mbili, pamoja na maendeleo endelevu kwa wananchi wetu. Kwa niaba yangu na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, napenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa mwaliko huu,” alisema Rais Samia.
Aidha, Rais Samia alikumbusha mchango mkubwa wa Urusi katika harakati za Tanzania za kupigania uhuru na kumpongeza Rais Putin kwa maadhimisho ya miaka 81 ya Ushindi katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia yaliyofanyika Mei 9 mwaka huu.
Rais Samia aliwasili Moscow kwa ziara yake ya kwanza nchini Urusi, ambayo pia ni ziara ya kwanza ya kiongozi wa Tanzania nchini humo katika kipindi cha zaidi ya miaka 50, kwa ajili ya mazungumzo na Rais Putin.
Viongozi hao kwa mujibu wao walijadili masuala mbalimbali yanayohusu kuimarisha zaidi uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Vilevile, walibadilishana mawazo kuhusu masuala muhimu yanayohusu ajenda za kimataifa na kikanda.










Comments
Post a Comment