Kufuatia kuongezeka kwa baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kupakia maudhui yanayokiuka maadili ya Kitanzania, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, amesema Serikali ipo katika hatua za mwisho kuja na mwarobaini wa kudhibiti tabia hiyo inayozidi kuathiri jamii hususan vijana.
Akizungumza kuhusu mwenendo wa maudhui kwenye majukwaa ya kidijitali, Waziri Makonda amesema umefika wakati sheria zichukue nafasi yake badala ya kuendelea kutoa onyo kwa maneno pekee.
Aidha, Serikali imewataka watumiaji wa mitandao ya kijamii pamoja na wanaojiita content creators kuhakikisha wanazingatia maadili, sheria na utu wa jamii wanayoiwakilisha mtandaoni huku hatua kali zikitarajiwa kuchukuliwa kwa watakaobainika kukiuka taratibu zilizowekwa.

Comments
Post a Comment