Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Esther Bulaya, ameungwa mkono bungeni kutokana na hoja nzito aliyowasilisha huku wabunge wakitoa pongezi kwa timu ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kwa historia waliyoandika usiku wa kuamkia leo Kwa kufuzu Fainali za AFCON 2026 na kukata Tiketi ya kushiriki Mashindano ya Kombe la Dunia la Vijana chini ya umri wa Miaka 17 Mwaka 2026.
Azimio hilo liliwasilishwa na Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Mhe. Esther Bulaya wakati wa Kikao cha 39 cha Mkutano wa 3 wa Bunge la 13, leo Mei 29, 2026 Jijini, Dodoma.
Akitoa pongezi kwa kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake binafsi katika kukuza michezo nchini na kuendeleza vipaji vya watoto wa Kitanzania, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda amesema hatua hizo zimeifanya Tanzania kuendelea kutambulika kimataifa kupitia mafanikio ya michezo.
Amesema uwekezaji mkubwa unaofanywa na Rais Samia katika sekta ya michezo ni matokeo ya maono na mapenzi yake ya dhati kwa vijana wa Tanzania, huku akibainisha kuwa wizara yenye dhamana ya habari, michezo na utamaduni sasa inaendelea kupata mafanikio makubwa kutokana na msukumo huo.



Comments
Post a Comment