Benki ya Azania imezindua rasmi huduma mpya ya malipo ya kidijitali ijulikanayo kama Azania Lipa, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza mkakati wake wa kuboresha huduma za kifedha kupitia teknolojia na kuleta urahisi zaidi kwa wateja wake.
Huduma ya Azania Lipa ni mfumo wa kisasa unaowawezesha wateja kufanya malipo kwa urahisi kupitia QR code, namba ya malipo (till number), pamoja na kutumia simu za mkononi kupitia Mobile Banking au USSD. Mfumo huu umeundwa kuunganisha huduma za benki, mitandao ya simu na wafanyabiashara katika jukwaa moja lenye ufanisi.
Uzinduzi wa Azania Lipa umeongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Ubunifu na Mikakati, Ndg. Jackson Lohay ( wanne kutoka kushoto)
Benki hiyo imewahimiza wafanyabiashara, wajasiriamali na wananchi kwa ujumla kuanza kutumia Azania Lipa ili kufurahia urahisi, usalama na ufanisi wa huduma hiyo mpya.
Uzinduzi wa Azania Lipa unaendelea kudhihirisha dhamira ya Benki ya Azania ya kuwa mstari wa mbele katika utoaji wa suluhisho bunifu za kifedha zinazokidhi mahitaji ya wateja na kuchangia maendeleo ya uchumi wa kidijitali nchini.








