Shirika la Reli Tanzania (TRC) lilianza kutoa huduma ya usafirishaji abiria kutumia reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) mnamo mwezi Juni 2024, toka kipindi hicho mpaka Machi 2026, abiria 5,512,995, wamesafiri kwa kutumia treni za SGR.
Takwimu hiyo ina ujumbe mkubwa sana kimkakati kuhusu ubora na mafanikio ya huduma ya SGR, na ina maana zifuatazo:
Kwanza ni Kukubalika kwa Huduma (High public acceptance)
Abiria zaidi ya milioni 5.5 ndani ya muda mfupi inaonyesha kuwa, Wananchi wameikubali kwa kiwango cha juu kabisa, huduma ya SGR kwani mejenga imani kubwa kwa watumiaji. Ukiachana na hilo, SGR imekuwa chaguo kuu la usafiri ukilinganisha na njia nyingine na usafiri na usafirishaji, lakini kubwq zaidi hii ni ishara ya market penetration yenye mafanikio makubwa.
Pili inadhihirisha Ufanisi wa Utoaji Huduma (Service Efficiency), na kwa muktadha huo, idadi hii inaashiria kuwa, huduma inapatikana kwa uhakika na ratiba zinazingatiwa , katika kipindi chote hicho uendeshaji umekuwa ni wa kuaminika (reliable), hili la pili lina maanisha kwamba ,TRC imefanikiwa kusimamia miundombinu na uendeshaji kwa ufanisi.
Tatu, ni kudhihirika kwa Ubora wa Huduma (Customer Experience), abiria kuendelea kutumia huduma hiyo kunamaanisha, wanaridhika na usalama, mwendo na faraja aidha kuna uzoefu mzuri wa safari (customer satisfaction), la tatu lina maanisha kwamba huduma hii mpya katika sekta ndogo ya reli nchini, imeleta thamani halisi kwa mtumiaji.
Nne, Mchango wa Kiuchumi na Kijamii, huduma hii ya treni za SGR, inachochea ukuaji wa uchumi (biashara, ajira na utalii) pia inarahisisha muunganiko wa mikoa (kati ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma) hili la nne linajipambanua kuwa kusafiri na treni za SGR, kunapunguza gharama na muda wa usafiri kwa wananchi.
Tano, haya ni Mafanikio ya Uwekezaji wa Serikali, na kwamba takwimu hizo za abiria katika kipindi cha muda mfupi wa huduma ya treni za SGR, inaonyesha kuwa, Uwekezaji wa Serikali kwenye SGR umeanza kuzaa matunda, kwa kuongeza huu ni mradi wenye tija (value for money) na unatekeleza dira ya maendeleo ya Taifa 2050 sambamba na Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2025/30, ambayo moja ya malengo yake ni kuimarisha miundombinu ya kisasa ya usafiri na usafirishaji
Hitimisho, idadi ya abiria zaidi ya milioni 5.5 waliotumia SGR ndani ya kipindi kifupi tangu kuanza kwa huduma inaonyesha kiwango kikubwa cha kukubalika kwa huduma hiyo, ufanisi wa uendeshaji, na mchango wake muhimu katika kurahisisha usafiri, kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.
