Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa 152 wa Umoja wa Mabunge Duniani unaoogozwa na Mheshimiwa Naibu Spika wa Bunge Mhe. Daniel Sillo (Mb) umekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa IPU na Spika wa Bunge Mstaafu Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) katika Hoteli ya Hilton Istanbul Bomonti Jijini Istanbul, Uturuki.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Sillo amewasilisha salamu za Spika wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) na kutambulisha Ujumbe wa Tanzania ulio pamoja nae kushiriki Mkutano huo unaotarajiwa kuanza rasmi tarehe 15 hadi 19 Aprili 2025, jijini humo.
Mhe Silo alieleza utayari wa Tanzania katika kuitangaza Tanzania kupitia fursa na vivutio vyake pamoja na kuwakaribisha Wajumbe wa Umoja wa Mabunge, kushiriki Mkutano wa 153 ambao Tanzania atakuwa Mwenyeji.
Aidha, utayari wa Wajumbe wapya wa Uwakilishi wa Tanzania katika kuhakikisha wanapata nafasi mnalimbali za uwakilishi ndani ya Umoja na kuendelea kuitekeleza sera ya diplomasia ya kibunge na kiuchumi.
Waheshimiwa Wabunge wawakililishi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mabunge Duniani ni Mhe. Bal. Dkt. Pindi Chana, Mhe. Elibariki Kingu, Mhe. Rashid Shangazi, Mhe. Fatma Rembo, Mhe. Asha Feouz, Mhe. Kiza Mayeye na Mhe. Dkt. Zeyana Abdallah Hamid.

.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
